Loading...
 

Uundaji wa Klabu- Kwanini Uanzishe Klabu

 

Kwanini uanzishe klabu?

Kuanzisha klabu ni jitihada ya kufurahisha ya kipekee:

  • Itakufundisha vitu vingi sana kuhusu uongozi. Hamna changamoto kubwa kama kuongoza jamii ya maofisa wa kujitolea, ambapo unatakiwa kujadiliana, kushawishi na kupanga majukumuu mara kwa mara.
  • Utakuwa unatengeneza matokeo ya muda mrefu na chanya kwenye maisha ya watu wengi. Tunahimiza kazi za nje ya klabu na kujihusisha kwenye uongozi wa miradi ya kweli kwenye jamii ambayo haihusiani na Agora. Tunataka wazungumzaji wa hadhira ambao tunawafunza kutoka na kwenda kuzungumza na viongozi ambao tunawafunza wawe na matokeo ya kweli na chanya kwenye dunia inayowazunguka. Na kwa kuunda klabu, utakuwa ni pointi ya kuanzia ya matokeo yote haya ya njia njema.
  • Utakuwa mmoja wa wanachama kwenye jamii ya kusisimua na yenye shauku. Baadhi ya watu utakaokutana nao na kuwaongoza wanaweza wakabadilika na kuwa mtandao wako wa mawasiliano ya kitaalam, au kuwa marafiki wa karibu.
  • Kwasababu Agora Speakers ni mpya kidogo, utakuwa labda unatengeneza historia kwenye mji wako au nchi yako na utatambuliwa kama mtu ambaye aliyeianzisha hapo. Unaweza pia ukahojiwa na redio au runinga, kama ambavyo imeshawatokea baadhi ya mabalozi.
  • Inaweza pia ikawa uthibitisho bora wa uwezo wako, unaweza ukapata nafasi za kitaalam au kazi zinazohusisha uongozi, usimamizi, au mawasiliano.

 

Agora Speakers Kota Kinabalu, nchini Malaysia
Agora Speakers Kota Kinabalu, nchini Malaysia

 

Kama unaanzisha klabu ya kwanza nchini au jimboni kwenu, unaweza pia ukataka kuomba kuwa balozi wa Agora. 

Kuanzisha mkutano, unahitaji:

  • Muda na nguvu kidogo.
  • Kuwa na japo watu 8 zaidi ambao wanavutiwa kukutana mara kwa mara. (Hii inawezekana kirahisi kwasababu kuna watu wengi ambao wanahitaji aina hii ya kujifunza)
  • Mahali pa mkutano (Isipokuwa kama una mpango wa kuwa klabu ya mtandaoni tu)
  • Kama hauna ujuzi na klabu au taasisi nyingine yoyote ya uzungumzaji mbele ya hadhira, mafunzo ya mtandaoni kidogo yatatolewa.

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Monday May 31, 2021 17:29:01 CEST by zahra.ak.